Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Khorramabad Iram, Hujjatul-Islam Behrouz Shamsi-Far, Imam wa muda wa Swala ya Ijumaa wa Khorramabad, katika khutuba za Swala ya Ijumaa ya wiki hii katika Msikiti wa Al-Ghadir wa mji huo, alisema: “Kuondoka wanajeshi wa Marekani nchini Iraq kumefikisha ujumbe wa ushindi duniank, na mashambulizi mazito ya Majeshi ya Iran dhidi ya kambi ya adui nchini Iraq yalisababisha Marekani kulazimika kuondoka. Siku itafika ambapo wataondoka katika eneo hili; hivyo, ushindi huu nchini Iraq ni matunda ya damu ya Shahidi Haji Qasim na Abu Mahdi Al-Muhandis.”
Alisema: “Kuondoka wanajeshi wa Marekani nchini Iraq kumeoesha kwamba; muqawama huu unaleta heshima na ni mfano kwa mataifa mengine duniani. Haipaswi kuruhusiwa makafiri kufikia malengo yao. Kusimama imara huku ndiko kulikoweka mazingira ya adui kukimbia, na huu ni ukombozi wa mataifa yaliyodhulumiwa kutoka katika dhuluma za maadui.”
Imam wa muda wa Swala ya Ijumaa wa Khorramabad alisisitiza: “Wananchi wa Iraq wanapaswa kuufikisha mwanzo huu hadi mwisho. Hata hivyo, katika masuala ya kiuchumi, Marekani bado ina ushawishi juu ya nchi hii. Kwa hiyo, muqawama wa Iraq unapaswa pia kupata uhuru wa kifedha, na hawapaswi kuruhusu makafiri kuwaamulia katika masuala ya kifedha.”
Hujjatul-Islam Shamsi-Far alisema: “Sehemu kubwa ya kambi za Marekani katika eneo hili zimekuwa hazina manufaa na hazifanyi kazi, na jambo hili limeweka mazingira ya wao kuondoka. Katika miongo miwili ya uwepo wa Marekani nchini Iraq, isipokuwa ukosefu wa usalama, kuundwa Daesh (ISIS), kuuawa wanasayansi na kuzuia maendeleo, hakuna jambo jingine lililofuatia, na popote walipo hawa, isipokuwa hasara na madhara, hakuna jambo jingine wanalolileta.”
Imam wa muda wa Swala ya Ijumaa wa Khorramabad, akizungumzia kumbukumbu ya mwaka ya Hamasi ya Tufani ya Al-Aqsa, alisema: “Mhimili wa muqawama umetoa gharama, lakini kupitia operesheni hii utawala wa Kizayuni uliwekwa katika mteremko wa kuanguka, na operesheni hii ilikuwa ya kipekee sana.”
Maoni yako